MTANZANIA WA KWANZA KWENYE GAZETI LA FORBES




Mfanaya biashara maarufu Tanzania amekua mtanzania wa kwanza kuwekwa picha yake katika gazeti maarufu la kibiashara Forbes, 

Mfanyabiashara huyo ajulikanae kama MO alionekana katika gazeti hilo maarufu katika mwezi wa July huku kukiwa na kichwa cha habari kilichosomeka “100 Hours a week, $ 85 million a year.”

kupitia mahojiano na Forbes mfanyabiashara huyo aliweka wazi kuwa alijiunga na Mohamed Interprises Tanzania Limited mwaka 1999 wakati mapato ya kampuni hiyo yalikua $ 26 million za kimarekani, 

Na sasa katika mwaka 2013, mapato  hayo yanakadiriwa kukua zaidi hadi kufikia zaidi ya dola billion moja za kimarekani, huku akikiri kuajiria watu zaidi ya 24,000. mapato hayo ya mfanyabiashara huyo yanakisiwa kuchangia karibu 3% ya GDP na Kuajiri karibu 5% ya ajira katika sekta Rasmi.

katika kilimo mfanyabiashara huyo anamiliki hekta 60000 za ardhi ya kilimo. huku akimiliki pia kiwanda kikubwa zaidi cha nguo katika ukanda wa sub-saharan afrika. 

Comments

Popular posts from this blog

KAMPUNI YA BF SUMA YAENDELEA KUGUSA MAISHA YA WATU TANZANIA

KIKOSI KIPYA CHA TAIFA STARS, CHINI YA KOCHA MPYA MZAWA.

SHBIKI WA ARSENAL APOTEZA NYUMBA, NI BAADA YA CLUB YAKE PENDWA KUSHINDWA.