MELI KUBWA ZAIDI YAWASILI BANDARI YA DAR ES SALAAM.















Meli kubwa ya mizigo yenye uwezo wa kubeba makontena 4500 ikiwa na urefu wa zaidi ya viwanja viwili vya mpira, imewasili ncini Tanzania katika bandari ya Dar Es Salaam, nakufanikiwa kuweka historia kwa meli za aina hiyo kuwasili hapa nchini, katika mahojiano aliyoyafanya Waziri mwakyembe amethibitisha ujio wa meli hiyo nakukiri kwamba ripoti kuhusu bandari hiyo kushindwa kukidhi meli kubwa si za kweli tena. 

Meli hiyo kubwa iliyopeperusha bendera ya Honkong, ilitia nanga katika bandari ya Dar, ikiongozwa na Kaptein wa Kitanzania ndugu Abdalah Mwongamno na kundi lake waliotumia muda wa siku kumi (10) kusafiri kutokea Lagos Nigeria mpaka Bandari ya Dar. 

Kufuatia kuwasili kwa meli hiyo kubwa, mamlaka zinazohusika zimeombwa kufanya kazi usiku na mchana ili kuhakikisha zoezi zima lakupakua mzigo linamalizika kwa haraka na ufanisi zaidi.

Comments

Popular posts from this blog

KAMPUNI YA BF SUMA YAENDELEA KUGUSA MAISHA YA WATU TANZANIA

KIKOSI KIPYA CHA TAIFA STARS, CHINI YA KOCHA MPYA MZAWA.

SHBIKI WA ARSENAL APOTEZA NYUMBA, NI BAADA YA CLUB YAKE PENDWA KUSHINDWA.