CHARLES TAYLOR KUTUMIKIA KIFUNGO CHAKE NCHINI UINGEREZA.
Rais wa zamani wa Liberia, Charles Tailor kupelekwa Uingereza kutumikia kifungo chake cha miaka 50, kwa makosa ya kiuka haki za binaamu, huku mahakama hiyo ikitupilia mbali ombi la watetezi wake la kuhamishia kifungo chake katika gereza la Rwanda ambako watuhumiwa wengi wa makosa ya jinai na ukiukwaji kwa haki za binadam wanatumikia.
Wakati mahakama hiyo ikikataa uezekano wa kumpeleka Charles Taylor nchini Rwanda na kwingineko huku ikitilia mkazo suala la kutumikia kifungo chake hukohuko Uingereza, Mataifa ya Afrika yanataraji kukutana muda mchache baadae kujadili kwa kina nafasi na ushiriki wao katika mahakama ya mashtaka ya umoja wa kimataifa, yenye makao yake huko The Hague.
Hata hivyo familia ya bwana Taylor imeandika barua kwa umoja wa Afrika huku ikiuomba umoja huo kushughulikia suala la Raisi huyo mstaafu wa liberia kutumikia kifungoo chake huko nchini Uingereza nakusisitiza kua Charles Taylor alitakiwa kutumikia kifungo chake katika ardhi ya Afrika na sio Ulaya kama ilivyopangwa. Mr urthur ambaye ni msemaji wa familia ya bwana Taylor alienda mbali zaidi nakubainisha kua familia kwa ujumla inahofia usalama wa Mr Taylor katika kutumikia kifungo chake nje ya nchi yake.
Comments
Post a Comment